Jeshi la polisi mkoani Mtwara linawashikilia watu sita wakiwa na magari
mawili ya mzigo ambao walijaribu kusafirisha tani 29 za korosho kupitia
bandari ya Mtwara zinazosadikika kuwa zimenunuliwa nje ya mfumo wa
stakabadhi gharani maarufu kama Kangomba.
Watu hao wamekamatwa bandarini jana majira ya saa mbili usiku wakiwa na vielelezo feki.
Jana majira ya saa mbili usiku dereva Bakari Seleman akiendesha lori
namba T 870 AHS likiwa limebeba magunia 150 pamoja na dereva Emanuel
Luckas akiendesha lori namba T 529 AJR likiwa limebeba magunia 220 ya
korosho,wakiwa na wafanyabiashara wawili wenye asili ya Asia pamoja na
wasaidizi wao,waliwasili geti namba tatu la bandari ya Mtwara kwa ajili
ya kupitisha mzigo huo ili uweze kusafirishwa.
Wafanyabiashara hao walikuwa na vielelezo bandia vya mzigo huo hali
ambayo ikawafanya kutiliwa mashaka na askari wa mamlaka ya bandarini.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mtwara ambae ni
mkuu wa mkoa huo Halima Dendego anasema haijalishi msimu wa korosho
unaelekea mwisho zoezi la kupambana na udhibiti wa kangomba bado
unaendelea.
Post a Comment