
Akisoma hati ya mashtaka mahakamani hapo mbele ya hakimu anayesikiliza
kesi hiyo, Anold Kirekiano mwendesha mashtaka wa polisi, Elisha Moleli
amesema mtuhumiwa huyo alitenda kosa la kuzini akijua kufanya hivyo ni
kosa la jinai.
Alisema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Januari 17 mwaka
huu nyumbani kwake mtaa wa Gezaulo majira ya saa 3:30 asubuhi kwa
kumwingilia kwa nguvu na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za
siri.
Mtuhumiwa huyo alikana shtaka hilo ambapo hakimu anayesikiliza kesi hiyo
aliharisha hadi Februari 9 mwaka huu itakapotajwa tena na mtuhumiwa
yupo rumande baada ya kushindwa masharti ya dhamana.
Post a Comment