Kamati za maji katika mitaa ya Kata ya Mlimani, Halmashauri ya Mji wa Handeni, zimetakiwa kuwasomea wananchi mapato na matumizi yatokanayo na mradi huo.
Akizungumza na wananchi waliojitokeza
kuunda kamati mpya ya maji ya Mtaa wa Kwasindi jana, Diwani wa kata hiyo,
Mwajabu Suphiani amesema tatizo la kamati nyingi hujisahau kuwa zimewekwa na
wananchi.
Amesema imekuwa desturi kila
kamati inayoundwa kukumbwa na tatizo la kushindwa kuwasomea wananchi
mapato na matumizi ya mradi, huku
wengine wakipingana na viongozi wao kuhusu uwazi wa matumizi ya fedha hizo ambazo ni za wananchi.
wengine wakipingana na viongozi wao kuhusu uwazi wa matumizi ya fedha hizo ambazo ni za wananchi.
Hivi karibuni, Mbunge wa Handeni
Mjini, Omari Kigoda ameagiza kama kamati hizo zimeshindwa kusoma mapato na matumizi
zivunjwe na ziundwe
nyingine.
nyingine.
Post a Comment