CHAMA Cha
Mapinduzi CCM Zanzibar kimesisitiza kuendelea kuisimamia Serikali kuu
kuhakikisha inatekeleza kwa vitendo ahadi zote ilizoahidi kwa wananchi.
Katibu wa
Idara Maalum ya NEC, Itikadi na Uenezi Zanzibar Waride Bakari Jabu ametoa ahadi
hiyo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari akiwapongeza wafuasi wa CCM na
wananchi wa jimbo la Dimani kufuatia ushindi wa chama hicho katika uchaguzi
mdogo wa ubunge uliofanyika jana.
Katika
pongezi zake, Waride Amesema ushindi wa mgombea wa Chama hicho katika uchaguzi
huo umekuwa mkubwa kuliko ule wa uchaguzi wa mwaka 2015, ishara inayotoa
matumaini ya kuwa wananchi wa jimbo hilo wanaendelea kuiunga mkono CCM.
Akizungumzia
tathimini ya CCM katika Uchaguzi huo amesema umefanyika katika mazingira
yaliyokuwa huru na Kidemokrasia kwa kuzingatia maelekezo na masharti ya
NEC yaliyotolewa kabla ya kuanza zoezi hilo.
Aidha
Waride ameahidi kuwa CCM itasimamia kikamilifu viongozi wake wanaotokana na
ridhaa za Wananchi hasa Wabunge, Wawakilishi na Madiwani ili waweze kutekeleza
Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho ya mwaka 2015/2020 kwa mujibu wa
mahitaji halisi ya wananchi.
Katika
uchaguzi uliofanyika jana Juma Ali Juma
amepata kura 4,860 na kumshinda mpinzani wake kutoka CUF, Abdulrazak Khatib
Ramadhan aliepata kura 1,234.
Post a Comment