Baraza
la madiwani la Halmashauri ya Musoma vijijini mkoani Mara limeagizwa
kuchukua hatua kali kwa uongozi wa kituo cha afya cha Murangi katika
halmashauri hiyo, baada ya kudaiwa kutumia gari la wagonjwa kufanya
biashara ya kubeba abaria na kusababisha gari hilo la kisasa kuharibika
katika kipindi kifupi baada ya kununuliwa.
Waziri
wa Nishati na madini ambaye pia ni Mbunge wa Musoma vijijini Mh Prof
Sospeter Muhongo,ametoa agizo hilo baada ya kukabidhi misaada ya vitu
mbalimbali zikiwemo baiskeli nne za kubebea wagonjwa na vitanda kumi
kwa ajili ya wagonjwa wanaolazwa katika kituo hicho kinachotumika hivi
sasa kama hospitali ya halmashauri ya wilaya na kuelezwa kuhusu
kuharibika kwa gari hilo.
Naye
mkuu wa wilaya ya Musoma Dk Vicent Naano, akizungumza baada ya Mbunge
huyo wa Musoma vijijini kutoa agizo hilo,amesema serikali itachukua
hatua kali kwa watu waliosababisha kuharibika kwa gari hilo la kisasa la
wagonjwa katika kituo hicho.
Post a Comment