MAKATIBU na Washika fedha Wa mfuko wa maendeleo ya majimbo Kisiwani Pemba wametakiwa kusimamia vizuri fedha zinazotolewa na Serikali kupitia mfuko huo katika kuhakikisha miradi wanayosimamia inatekelezeka.
Ushauri huo umetolewa na Naibu waziri Ofisi
ya Makamo wa pili wa rais Mhe. Mihayo Juma Nhunga alipokuwa akifunguwa mafunzo
ya siku moja kwa makatibu, wakurugenzi na washika fedha wa mfuko wa
maendeleo ya jimbo huko katika ukumbi wa Tassaf.
waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Mhe Mihayo Juma akifungua
mafunzo ya siku moja watendaji wakuu wa Mfuko wa Jimbo Kisiwani Pemba.
Amesema katika awamu iliyopita fedha
hizo hazikutumika vizuri katika utekelezaji wa miradi mbali mbali ndani
ya majimbo hali ambayo wasimamizi walishindwa kuwasilisha
ripoti ya matumizi ya fedha za miradi hiyo.
Nae Mkurugenzi Uratibu wa Ofisi ya
Makamo wa pili wa Rais Nd,Khalid Bakar Hamad na Afisa Mdhamini wa Ofisi
hiyo Ali Salim Matta wamesema fedha hizo zinazotolewa na Serikali
sio sadaka na badala yake zitumike katika kuwaletea wanachi
maendeleo majimboni.
Post a Comment