Na mwanishi wetu Zanzibar
AFISA Mdhamini Wizara ya Afya Pemba Bakar Ali
Bakar amebaini kuwepo na upotevu wa mashuka 36 na mito 20 katika
Hospitali ya Wete na kuuagiza uongozi wa hospitali hiyo kuhakikisha
vifaa hivyo vinapatikana ndani ya kipindi cha wiki mbili.
Amesema upotevu wa mashuka na mito hiyo
ameubaini kufuatia ziara yake ya kukagua utoaji wa huduma kwa
wagonjwa katika hospitali hiyo ambapo alipokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa
juu ya ubovu wa mashuka katika vitanda vya wodi ya watoto.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana
Ofisini kwake ,Bakar amesema ziara hiyo aliyoifanya akiwa
ameambatana na maafisa wa Wizara hiyo Pemba , alishuhudia vitanda
vikiwa na mashuka machakavu.
Ameeleza kwamba hali hiyo ilimfanya ahoji
sababu zinazowafanya kuendelea kutumia
mashuka yaliyochakaa licha ya Serikali kuandaa mazingira mazuri
ya upatikanaji huduma bora kwa wagonjwa ikiwemo suala la malazi.
Post a Comment