Na Mwandishi wetu zanzibar
Ofisi
ya Mufti Zanzibar imeliomba Jeshi la
Polisi Zanzibar kumchukulia hatua za kisheria kijana Abdalla Saleh
anaedaiwa kutoa matamshi ya kumkashifu Mtume Muhammad (s.a.w).
Mufti Mkuu wa Zanzibar
Sheikh Saleh Omar Kaabi
Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa
habari ofisini kwake Mazizini Mjini Unguja Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi amesema
matamshi yaliyotolewa na kijana huyo yanaweza kuvuruga amani ya nchi na
kuharibu uhusiano wa Zanzibar kimataifa.
Pamoja na hayo, mufti mkuu ametoa onyo kwa
waumini wa dini hiyo kutokutowa maneno
yenye kuikashifu imani yao.
Aidha amewasihi waislamu
wote kuwa watulivu na kusubiri vyombo vya kisheria kumchukulia hatua kijana
huyo
Post a Comment