0

 


NB-Picha haihusiani na habari hapa chini

Watu watano wamefariki dunia na sita kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na mwamba wa mawe katika shimo la mgodi wa zamani wa Resolute Nzega mkoani Tabora.


 Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea baada ya kundi la wachimbaji wadogo wa mgodi wa Umoja kuvamia eneo hilo ambalo limepigwa marufuku na serikali.

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa wilaya ya Nzega Godfrey Ngupulla amesema eneo hilo limezuiwa kuchimbwa kutokana na hatari iliyopo lakini baadhi ya wachimbaji wamekuwa wakiingia kwa kificho kuchimba.

Amewataja walipoteza maisha kuwa ni Joseph Mpenda,mkazi wa Shinyanga,Mohamed Mohamed,mkazi wa Singida,Manona Nyombi,mkazi wa Bariadi na Modesta Leonard,mkazi wa  Nzega.

Waliojeruhiwa ni Kang'wa Mayenga,mkazi wa Bariadi,Agnes Anthony,mkazi wa Chato,Deus Alponce,mkazi wa Igunga na aliyefahamika kwa jina moja la Mapunda mkazi wa Chato.

Post a Comment

 
Top