
Mara nyingi tumekuwa tukisikia juu ya vipodozi bandia au dawa bandia lakini masuala yanayohusu chakula bandia hayakuwa yakigonga vichwa vya habari sana hadi hivi karibuni dunia ilipopata mshtuko juu ya uwepo wa mchele wa bandia.
Mchele huu wa bandia ambao umekuwa ukihatarisha afya za watu wengi
hufanana sana na mchele wa kawaida kiasi kwamba ukiiangalia kwa macho
huwezi kuutofautisha.
Mchele huu unaosambaa kwa kasi duniani hutengenezwa kwa plastiki na
utofauti wake na mchele wa asili huonekana mara baada ya kuupika.
Jana, mamlaka katika mji wa Lagos nchini Nigeria ilikamata magunia 102
ya mchele wa plastiki yaliyokuwa yanaingizwa nchini humo na
wafanyabiashara haramu ambao walitaka kuuza katika msimu huu wa sikukuu
ili kujipatia fedha nyingi zaidi.
Nigeria inaendelea na uchunguzi kutambua ni kiwango gani cha mchele huo
kimekuwa kikiuzwa na ni vipi unaweza kuondolewa sokoni ili kulinda afya
za raia wa Nigeria waliokwisha utumia na kuwapeleka wahusika wa
biashara hiyo haramu mbele ya sheria
Mchele huu umeelezwa kuwa ni hatari sana kwa afya ya binadamu kwani ni
sawa na kumlisha mtu plastiki lakini pia wingi wa kemikali zinazotumika
katika utengenezaji wa mchele huo.
China imedaiwa kuwa ndiyo nchini inayoongoza kwa utengenezaji wa mchele huu.
Post a Comment