Wabunge wa upinzani nchini Kenya wametoka bungeni kwa hasira katika mji
mkuu wa Nairobi, wakisema kuwa baadhi yao walinyanyaswa bungeni mapema
asubuhi.
Kikao hicho maalum ambacho vyombo vya habari havikuruhusiwa kuingia
kilitarajiwa kupigia kura marekebisho ya sheria ya uchaguzi ambayo
inaruhusu kuhesabiwa kwa kura moja baada ya nyengine katika uchaguzi wa
urais mwaka ujao.
Serikali inataka mfumo ambao utasaidia shughuli ya kuhesabu kura iwapo
mfumo wa kielektroniki utafeli lakini upinzani unasema kuwa ni njia moja
ya kuiba kura.
Awali hatua ya kuupigia kura mswada huo ili ufanyiwe marekebisho ilisababisha kuzuka kwa ghasia siku ya Jumanne.
Upinzani wa CORD umesema kuwa mmoja ya wabunge wake alivuja damu usoni
kufuatia mgogoro na wabunge wa chama tawala mapema siku ya Jumatano.
Cord imeenda mahakamani ikitaka marekebisho hayo kutopitishwa bungeni lakini chama tawala kimepitisha marekebisho hayo.
Via>>BBC
Post a Comment