0


Na mwanishi wetu                                                        
Mbunge wa Chaliinze Mkoani Pwani Ridhwan Jakaya  Kikwete amesema haifurahishi kuwashudia watazamia wenyewe kwa wenyewe wakipigana mikuki , kutoana raho au kumwagana damu bila sababu za msingi .
 Mh Mbunge wa Jimbo la  Chaliinze Mkoani Pwani Ridhwan Jakaya  Kikwete  



Jakaya ameyaeleza hayo jana mjini chalinze wakati alipozunguumza na wananchi wa jimbo hilo katika kijiji cha Bwilingu kata ya chalinze  wilayani Bagamayo.

mkulima aliyechomwa mkuki na mfugaji wiki iliyomalizika mikumi Mkoani  Morogoro  

Alisema hayo wakati akionesha masikitiki yake kwa wananchi wa jimbo lake juu ya tuki0 lililotokea tarehe 25 katika jimbo la Mikumi Mkoani Morogoro baada mkulima mmoja kupigwa mkuki na mfugaji uliongilia mdomoni na kutokea shingoni ambapo amesema kitendo hicho ni kinyume kabisa na ustaarabu wa watanzania wanaoishi kwa upendo, umoja na mshikamano .

"Wabunge tunaposimama bungeni na kueleza wapo wakulima  wamevunjwa  migongo , kupigwa mshale na kupata ulemavu , wapo wanaodhani tunatania , tukio hili liipe undisho Serikali , ije na majibu sahihi na   mkakati wa kunusuru  mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yasiendelee " Alisema Kikwete  .
Alisema kitendo cha  mtu kuvunjwa mgongo na kupigwa mkuki wa mdomo kutokea shingoni ni mambo  ya kuhuzunisha hivyo akaitaka serikali kuchukua hatua za haraka na kuhakikisha mivutano ya aina hiyo inamamalizika  kati ya wakulima na wafugaji.
"Serikali iwe sikivu na  sasa ije na utatuzi  wa kudumu kabla damu ya watanzania wanyonge wanaotegemea kilimo kama kiinua mgongo  , wasiendelee kupoteza maisha, sheria ya mipango na matumizi bora ya Ardhi itumike kumaliza utata huu  "Alisema
Aidha Jakaya alisema matatizo hayo yalioanza huko maeneo ya  Kilosa, Mvomero, Chalinze, Handeni,Kibaya  Kiteto na sasa Mikumi ameitaka   Serikali iamke na kujipanga  kabla mauaji na vifo havijaongezeka ..

Jakaya alisema iwe ni aibu na mwiko kwa mtanzania kuinua silaha ya aina yoyote kwa dhamira ya kutaka kumshambulia au kumdhuru mwenzake na kwamba atakayefanya hivyo sheria ichuke mkondo wake.

Post a Comment

 
Top