0



MKUU wa Wilaya ya Wete Kisiwani Pemba Mh .Rashid Hadid amesema  wananchi wa zanzibar wa kina kila sababu ya kujivunia mafanikio yaliyopatikana baada ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 kwa kuimarishwa huduma muhimu za kijamii .

        Amesema kwamba serikali imekuwa ikitekeleza kwa vitendo azma ya Mapinduzi hayo kwa kuhakikisha huduma za kijamii zinawafikia karibu na maeneo wanayoishi mijini na vijijini na bila ubaguzi wa aina yoyote .

       Akizungumza na wafanyakazi wa Idara , Taasisi  na Mashirika ya Umma baada ya kumalizika zoezi la usafi wa Mazingira katika Mji wa Wete , ikiwa ni shamra shamra za kutimia miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar, amesema  Serikali itaendelea kuboresha huduma hizo ili kila mwananchi aweze kunufaika na uwepo wake.

      Mkuu huyo wa Wilaya amesema Huduma za Maji, Umeme, Afya na Mawasiliano zimeboreka katika Wilaya hiyo na kukiri kuwepo sehemu chache ambazo hazijafikiwa na huduma hizo ambapo juhusi za kufikisha zinachukuliwa na Serikali .

       Aidha amewataka wafanyakazi hao kushirikiana na Serikali kupiga vita matendo ya udhalilishaji wa kijinsia ambayo yanaonekana kukithiri katika Wilaya hiyo.

Post a Comment

 
Top