0


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza walimu wanaoishi mbali na shule hali yakuwa shule zao zina majengo wahame mara moja na kuishi karibu na maeneo yao ya kazi

Amesema haifai kuacha walimu waishi mbali na maeneo ya shule kwani hali hiyo inachangia uchelewaji kazini na inapunguza muda wa kuwasimamia wanafunzi au kuwasaidia jioni pale wanapohitajika kufanya hivyo.

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Chingumbwa, kata ya Mbekenyera, wilayani Ruangwa kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi kijijini hapo.

Pia Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Andrea Chezue asimamie zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha anapunguza walimu walioko Ruangwa mjini na kuwahamishia shule za vijijini ambako kuna upungufu wa walimu.

Post a Comment

 
Top