Mkuu wa Wilaya ya Wete Rashid
Khadidi Rashid amewataka madaktari wa Wilaya ya hiyo kuendelea kutoa huduma
bora kwa mama wajawazito na mtoto ili kujiongezea sifa.
Mkuu wa Wilaya ya Wete Kisiwani Pemba Rashid
Khadidi Rashid(kulia)
Amesema hatua ya hospitali
ya Wete kupata ushindi wa kwanza katika utowaji wa huduma ya mama wajawazito na
watoto ni ya kupongezwa kwani ni miongoni mwa mikakati ya serikali ya kupambana
na vifo vya mama na watoto.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa wito huo katika ukumbi wa Benjameni Mkapa Wete kwenye sherehe za kupongezana kwa madaktari walioshiriki katika utowaji wa huduma hiyo kwa kupata washindi wa kwanza kwa hospitali zilizotekeleza mradi huo Unguja na Pemba.
Aidha amewataka madaktari hao kua mfano bora katika utoaji wa huduma za afya kwa jamii ikiwa ni pamoja na kutumia lugha nzuri wakati wa kuwahudumia wagonjwa ili wafurahie huduma zao.
Nae daktari Mkuu kisiwani Pemba Mbwana Shoka amesema pamoja na uchache wa madaktari lakini wameweza kufanikiwa kutoa huduma ya mama na mtoto na kupata ushindi wa kwanza kati ya hospitali nane za Zanzibar zilizoshiki katika
Post a Comment