0


Waziri  wa  nchi ya  ofisi ya  makamo  wa  pili  wa  Rais Zanzibar  Mohammed  Aboud ametoa tamko  rasmi  la  kuanza  kwa  sherehe  za  mapinduzi  matukufu  ya 53 ya zanzibar .


Akizungumza  na  waandishi wa habari ofisini  kwake vuga  mjin  Zanzibar, Mhe.  Aboud  amesema shamrashamra  hizo  zitaanzia  kesho  ambapo kutafanyika  shughuli  ya  usafi nchini  ikifuatiwa na Januari Mosi ambapo  Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein atawaongoza wananchi  katika mazoezi ya viungo kutembea.
        Miradi mbali mbali itazinduliwa kuelekea kilele cha sherehe za Mapinduzi Zanzibar Januari 12 mwakani, ikiwemo barabara ya Kwerekwe - Fuoni, sacoss ya  meli nne  wilaya  ya  magharib, kituo  cha  zimamoto  kilichopo  uanja wa ndege na  pia  kuwekwa  jiwe  la  msingi  katika  nyumba  za  zssf.

Post a Comment

 
Top