Na Amina Kibwana-Globu ya Jamii
Serikali ya Tanzania imepokea pokea
msaada wa hundi ya dola 50,000 (Dola elfu hamsini) kutoka katika ubalozi wa jamuhuri ya Korea kwa ajili ya
kukabiliana na athari zilizotokana na tetemeko
la ardhi Mkoani Kagaera, ili kuweza kurekebisha Miundo mbinu,makazi ya watu
pamoja na shule.
Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa mambo ya nje na
ushirikiano wa Afrika mashariki kikanda na Kitaifa Dk.Augustine Mahinga amesema
serikari ya korea ni mdau mkubwa hasa ktk
misaada ya kimaendeleo, kiuchumi ,
ustawi wa jamii na katika misaada ya kibinadamu ikiwa ni pamoja kusimamia
ujenzi wa hospitali ya logazila na chanika.
“Tumekuwa tukipokea misaada mbalimbali kutoka kwa marafiki
lakini huu ni mchanngo wa hivi karibuni kutoka kwa wenzetu wa korea ambapo leo nimepokea hundi hii kwa niamba ya
waziri mkuu na serikali ya Tanzania kwa ujumla.”
Hata hivyo Dk mahinga aliongeza kuwa hundi hiyo ni zawadi
kubwa kwa wanachi wetu hasa wa kagera pamoja
na kutoa shukrani zake kwa balozi wa korea na kuahidi kuwa kuendelea kufanya kazi kwa pamoja.
Kwa upande wake balozi wa jamuhuri ya korea song Young
amesema kuwa kutokana na ushirikiano wao wa muda mrefu Korea imeamua kutoa
msaada huo, Korea imeamua kwamba katika kuendeleza ushirikiano wa maendeleo na
nchi za afrika Tanzania itapewa kipaumbele na kuwa ni chi ya kwanza kwa afrika ili
kudumisha ushirikiano kati ya Jamuhuri ya Korea na tanzania.
huu ni mwaka wa 25 tangu
jamuhuri ya korea kuanzisha ubalozi wao nchini Tanzania,ambapo ili kudumisha
ushirikiano huo, Serikali ya Tanzania
kupitia Rais wake Dk John Pombe Magufuli nayo inatarajia kuanzisha ubalozi wake huko
soo mji mkuu wa korea kusini mapema mwaka 2017.
Post a Comment