Viongozi wa Japan na Marekani
Waziri Mkuu wa
Japan Shinzo Abe ametoa salamu za rambirambi kwa Wahanga wa shambulio
lililofanywa na nchi yake katika Bandari ya Pearl, nchini Marekani,
miaka sabini na tano iliyopita.
Akizungumza katika hafla
iliyoandaliwa kwenye kituo cha jeshi la majini la Marekani akiwa
sambamba na mwenyeji wake Rais Barak Obama, Bwana Abe amekiri kukosa la
kusema kutokana na uzito wa ziara yake katika kumbukumbu ya wale wote
waliopoteza maisha kutokana na shambulio hilo.
Ameishukuru Marekani kwa uvumilivu wake na kuongeza kuwa kitisho cha vita hakitajirudia kamwe.
Naye
Rais Obama kwa upande wake ameitaja ziara hiyo ya Waziri mkuu wa Japan
kuwa ni ya kihistoria na kusema kuwa inakumbusha kuwa hata maumivu
makubwa yaliyotokana na vita yanaweza kuleta urafiki na amani ya kudumu.
Amesema baada ya vita mahusiano yao yamekuwa ya amani na nchi zilizokuwa katika ukanda wa Asia Pacifik.
Miezi
saba iliyopita viongozi hao wawili walitembelea pia mji wa Japan,
Hiroshima, ambako Marekani uliushambulia kwa mabomu ya nyuklia.
Post a Comment