Ligi ya jogoo imeendelea tena leo desemba 14 kati ya timu ya kwa ngupili (hawili fc) dhidi ya toto sinza mchezo uliopigwa uwanja wa shule ya msingi mbaya.
Katika mchezo huyo timu ya Hawili fc imeweza kuzima ndoto za ubingwa wa timu ya toto sinza kwa kuichapa magoli 4-1
Katika kipindi cha kwanza timu ya Hawili fc iliweza kuongoza magoli 3 na toto sinza ilipata goli 1na kipindi cha pili Hawili fc iliongeza goli la 4 lililofungwa kwa mkwaju wa penaiti
Timu ya toto sinza katika mchezo wake wa desemba 12 ilishinda 7-2 dhidi ya kwa mchweke fc
Kwa msimamo wa ligi hii Timu ya Hawili fc ina pointi 4,toto sinza fc ina pointi 3,wakota fc ina pointi 1 na kwa mchweke fc inashika mkia haina pointi
Post a Comment