Ligi ya Jogoo kwa watoto chini ya miaka 12 imeanza kutimua vumbi desemba 11 kati ya timu ya Wakota fc dhidi ya kwa Ngupili fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa shule ya msingi Mbaya kata ya Mbaya wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
katika mchezo huo wa ufunguzi matokeo yalikuwa sare ya kufungana goli 2-2 katika mchezo huo timu ya kwa Ngupili ilikuwa ya kuwanza kufumania nyavu katika kipindi cha kwanza lakini baaada ya dakika 5 timu ya Wakota iliweza kusawazisha mapaka mapumziko ya dakika 45 ilikuwa sare ya goli 1-1.
Katika ligi hiyo kuna jumla ya timu 4 zilizothibitisha kushiriki ambazo ni Wakota f, kwa Ngupili fc,Toto Sinza fc na Mchweke fc
Kwa mujibu wa mratibu wa mashindano,Seif Kimbwanda alisema lengo kuu ni kukuza vipaji vya watoto pamoja na kujenga ushirikiano wa watoto baina ya vijiji jirani kati ya kijiji kipya cha Namtumbwa na kijiji cha Mbaya.
Kimbwanda aliongeza kusema anawaomba wadau mbalimbali wa soka kujitokeza kuweza kuwafadhili ili kuweza kukuza vipaji wa watoto vijijini akieleza kuwa michezo kwa watoto ina faida kubwa ikiwa kuwajenga kiakili licha ya kufanyika mashindano hayo lakini kuna changamotoya vifaa kama vile jezi na mpira,
Desemba 12 kulikuwa na mchezo mkali ya timu ya Toto Sinza fc dhidi ya kwa Mchweke fc mchezo ulimalizika kwa timu ya Toto Sinza kuweza kuibuka na ushindi mnono wa magoli 7-2
Post a Comment