Wakulima
na wafugaji hao ktk maeneo hayo wamezungumza kuwa muwekezaji huyo
amekuwa mara kwa mara akichepusha maji yam to Balali ambayo yanapashwa
kutiririka ktk mto Ruaha Mkuu na hivyo kuathiri kwa sehemu kubwa maisha
yao kwani wamekuwa wakikosa maji ya kwa ajili ya matumizi ya majumbani
na ya kuendeshea kilimo na ufugaji.
Kwa
upande wake Diwani wa kata ya Imalasongwe Bw Chuki Jeremiah anakiri
kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kutokana na kukosekana kwa maji
wakulima na wafugaji hao wamekuwa wakivutana na muwekezaji huyo kwa muda
sasa hali ambayo ktk siku za hivi karibuni imepelekea mauaji.
Afisa
wa Maji wa Bodi ya Maji ya Bonde la Rufiji Bw Idrisa Msuya amesema
amepokea malalamiko hayo na hivyo kumuagiza muwekezaji huyo kufuata
utaratibu uliopo kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa
dhidi yake.