Uongozi
wa wachama cha wananchi (CUF ) mkoa wa Kusini Pemba umesema hawaitambui
ziara ya Profesa Ibrahimu Lipumba kisiwani Pemba ki chama kwani
haiandaliwi na uongozi wa chama hicho mkoani humo na badala yake
wamemtaka aende kama Mtanzania.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa ulinzi na usalma wa chama hicho mkoa
wa Kusini Pemba Yusufu Salim Hussen ambae pia nimbunge wa jimbo la
chambani wakati alipokuwa akitowa taarifa kwa vyombo vya habari na
viongozi wa majimbo na wa wilaya Chake na Mkoani.
Wakizungumza
kisiwani Pemba baadhi ya wanachama wachama CUF kisiwani Pemba wamesema
Profesa Lipumba nimtanzania na hazuiwikuja Pemba kwa vile anahaki sawana
mtanzania yeyote ila hawata kubali kuzungumzanae katika masuala ya
chama.
Uongozi
wa CUF mkoa Kusini Pemba wamefanya mkutano huo kufatia tetesi zilizo
zagaa kisiwani Pemba kuwepo ziara ya Profesa Ibrahimu Lipumba hivi
karibuni.
Chanzo:ITV
