Siku moja baada ya Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako kusema waandishi waliomuandika vibaya watakufa kabla ya Machi 2017, Jeshi la Polisi linatarajia kutoa msimamo wake dhidi ya kauli hiyo leo.
Kauli
hiyo ya Mzee wa Upako aliyoitoa juzi kanisani kwake, ilikuwa ni
mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo akijibu
yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu madai ya kulewa na
kumfanyia fujo jirani.
Kamanda
wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro
jana alisema ni mapema kuzungumzia sakata hilo kwa sababu jana ilikuwa
sikukuu na atatolea ufafanuzi leo.
“Anasema
hao waandishi watakufa kabla ya Machi 2017 kwani yeye Mungu? Hilo ni
suala zito, tumeandaa mkutano na waandishi wa habari tutalizungumzia
suala hilo kesho (leo),” alisema Kamanda Sirro.
Katika
kauli hiyo, Mzee wa Upako alisema kila mwandishi aliyemuandika vibaya
ikifika Machi mwakani hatakuwa hai na kama wataendelea kuishi, ataacha
kazi ya kuhubiri injili na kwenda kuuza gongo.
Post a Comment