0


Benki ya Kimataifa ya Exim ya Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China  imeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kusaidia Maendeleo ya Wananchi wake kupitia miradi tofauti inayoanzishwa.


Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo Bwana Sun Ping wakati wa mazungumzo yake  na  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi anayeuongoza Ujumbe wa Viongozi Wanne wa Serikali akimalizia ziara yake ya Kiserikali ya Siku Tano Nchini China.
 makamo wa pili wa raisi serikali ya mapinduzi Zanzibar balozi Seifu ali iddi

 Bwana Sun Ping  amesema Taasisi hiyo ya Fedha ya China imeridhika na hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa na Zanzibar katika kuimarisha uchumi wake kiasi kwamba Benki hiyo itaangalia namna  za kusaidia nguvu katika kuona miradi inayoanzishwa inatekelezwa.
Makamu wa Rais wa Benki hiyo ya Exim alimueleza Balozi Seif na Ujumbe wake kwamba Tanzania  ndio nchi pekee iliyopewa kipaumbele na benki hiyo katika kupatiwa mikopo na misaada ikilinganishwa na Nchi nyengine Barani Afrika.   
    
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliipongeza Benki hiyo ya Exim kwa ukarimu wake wa kuunga mkono miradi ya Maendeleo inatotekelezwa Zanzibar kwa njia ya misaada na hata mikopo.
Balozi Seif amesema yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana  miongoni mwa Wanachi waliowengi Zanzibar  kufuatia kuibuka kwa miradi kadhaa ya Kiuchumi na maendeleo iliyopata msukumo kupitia Benki hiyo ya Kimataifa ya Exim.

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top