Na Mahmoud Ahmad Arusha
MKUU
wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti Amepata aibu baada ya kuzomewa
mbele ya Waziri wa Ardhi maendeleo ya makazi William Lukuvi katika ofisi
za mkuu wa mkoa wa Arusha .
Mnyeti alizomewa wakati akitoka katika kikao cha waziri kupewa taarifa za matatizo ya Ardhi mkoa wa Arusha.
Amezomewa Mnyeti kufuatia kitendo chake cha kuagiza kuwekwa rumande mwandishi wa ITV Halfani Liundi.
Agizo
hilo ambalo mpaka sasa lina ukakasi wa u halali wake kwa kua Lihundi
siyo makazi wa Arumeru anapotawala Mnyeti limelaaniwa na wadau wote wa
habari.
Ziara ya Lukuvi.
Waziri
Lukuvi amelazimika kufika Arusha kushughulikia kukithiri kwa migogoro
ya Ardhi hususani Wilaya ya Arumeru na viongozi wa Wilaya hiyo Kushindwa
kuyapatia ufumbuzi.
Hivi
karibuni Waziri mkuu akiwa katika ziara mkoani Arusha akiwa Wilaya ya
Arumeru alipokelewa na mabango ya wananchi wakilalamikia migogoro ya
Ardhi iliyokithiri Wilayani humo.
Katika
majumuisho ya ziara yake hiyo Waziri mkuu kasimu Majaliwa akaeleza kuwa
ukiona kiongozi wa juu anapokelewa na mabango katika Wilaya yenye
viongozi ujue kiongozi aliyopo hapo hatoshi.
Mwandishi Lihundi hadi Jana mchana alikuwa akihojiwa kituo cha polisi User River ili waweze kupata fursa ya kupata dhamana.
Aidha
kulikuwa na utata juu ya tuhuma zinazomkabili ambapo Mara baada ya
kufika mwanasheria anayemtetea katika kadhia hiyo Edwin Silayo kutaka
kuongea na Mteja wake mkuu wa upelelezi Wilaya alimzuia akidai Lihundi
hana kesi Bali amewekwa ndani kwa agizo la Dc.
Hali
hiyo ilizidi kuonyesha mkanganyiko kwa waandishi wa habari waliokuwepo
kituoni hapo na kulazimika kujiandaa vyema kushughulikia tatizo hilo.

Post a Comment