Imeelezwa
kuwa, kuwepo kwa taasisi ya
tume ya maadili
ya viongozi wa umma Zanzibar
kutasaidia kulinda maadili kwa
viongozi pamoja na
wananchi wake.
Mwenyekiti wa tume ya
maadili ya viongozi wa umma Zanzibar
Asaa Ahmad Rashid
Mwenyekiti
wa tume hiyo Asaa Ahmad Rashid ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake Shangani mjini Zanzibar, amesema kuundwa kwa
tume hiyo ni moja kati ya malengo ya Serikali na kuunda taasisi tofauti za
uwajibikaji na utawala bora.
Ameyataja baadhi
ya majukumu ya
tume hiyo kuwa ni pamoja na
kupokea malalamiko kutoka
kwa wananchi kuhusiana na
suala la uvunjifu
wa maadili lakini pia kukuza uelewa
wa maadili kwa
viongozi na wananchi.
Pamoja
na hayo Asaa ameweka wazi kuwa tume hiyo imeweka adhabu ya kukatwa mshahara,
kushushwa cheo, kusimamishwa kazi, kustaafishwa, kuondolewa madarakani au
kufukuzwa kazi kwa kiongozi wa umma atakaekiuka maadili yaliyowekwa na tume
hiyo.
Kwa
mujibu wa utaratibu wa tume hiyo, mwezi Disemba kila mwaka viongozi wa umma
wanatakiwa kujaza fomu maalumu ya tume hiyo na kuirudisha.
Tume hiyo
imeundwa na mwenyekiti
na makamishna wawili
akiwemo Said Bakari
Jecha na Sebtuu Mohammed Nassor.
Post a Comment