0


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kukubali maombi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuongeza bei ya umeme kwa asilimia 8.5 ifikapo januari mwaka 2017.

   Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji, EWURA, imetangaza ongezeko hilo  la bei  kwa asilimia 8.5 Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngalamgosi, amesema, ongezeko hilo la bei ni kufuatia maombi ya Shirika la Umeme Nchini, TANESCO, kutaka ongezeko la bei kwa asilimia 18.19, ifikapo Januari mwaka 2017.

Akitangaza bei hizo mpya jijini Dar es Salaam, leo Ngalamgosi amesema, baada ya kufanya uchambuzi wa kina, Mamlaka yake imefikia uamuzi wa kuongeza asilimia 8.5 itakayoanza kutumika Januari Mosi, 2017 kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wake.

Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) ambalo linanunua umeme wa jumla kupeleka Zanzibar limeongezewa kwa asilimia 5.7% ya bei ya umeme.

Hata hivyo ongezeko hilo halitaathiri wateja wa majumbani ambao matumizi yao hayazidi uniti 75 kwa mwezi.




Post a Comment

 
Top