Kuna msemo
unaosema Uzee mwisho Chalinze, msemo uliovuma sana kipindi cha nyuma
hata hivyo msemo huo umeweza kujitokeza tena mchana wa jana 23 Desemba
baada ya kutokea tafrani ndani ya basi la Mwendokasi (UDART) kwa wazee
wawili kupishana kauli na kisha kuamua kushikana mashati.
Tukio hilo la aina yake, lilinzia kituo cha Magomeni Morocco ambapo
abiria hao waliopandia basi lao hilo katika kituo hicho cha Magomeni kwa
mmoja wapo kumkanyaga mwenzie na hali ikabadilika ghafla na kuanza
kushikana mashati na kupigana
Wazee hao kila mmoja aliwa akimtambia mwenzie “Mimi huniwezi mtu wa
mjini nimesoma mjini Azania Boys!” na Mzee Mwingine akajibu mapigo kuwa
naye ni mtu wa mjini na amesoma mjini Tambaza Boys”.
Wazee ambao ni abiria na kila mmoja hakiwa na munkali, waliamua
kuvaana na kuanza kupigana makonde hadi abiria wengie walipowaamulia.
Post a Comment