Polisi nchini Kenya
katika jiji kuu Nairobi wamemkamata mlinzi wa Benki ya Equity kuhusiana
na wizi mwishoni mwa wiki ambapo wezi walitoweka na mtambo wa kutoa
pesa, ATM.
Wezi hao walitoweka na kiasi cha pesa ambacho hakijajulikana kwa sasa wakati wa wizi huo Jumamosi.
Wezi
hao walichimba ukuta wa nyuma wa Benki hiyo na kutoweka na sanduku la
uhifadhi wa pesa pamoja na mtambo wa ATM, pesa zikiwa ndani.
Washukiwa waliweza kuzima kamera za CCTV na pia kengele ya usalama kabla ya kutekeleza wizi huo.
Akizungumza
na BBC, kamanda wa jimbo la Nairobi Japheth Koome amesema kwamba polisi
waliweza kupata mitungi ya gesi na vifaa vingine ambavyo hutumuka
kukata chuma.
Alipoulizwa kama wezi siku hizi wamepata umaarifa
utadhani wanaiga filamu, alisema kwamba kwa siku za hivi karibuni wizi
wa benki unazidi kubadilika sana.
Mwaka uliopita, wezi waliojifanya wakaguzi wa hesabu katika benki hiyo walitoweka na dola za Marekani 300,000.
Post a Comment