Mgombea wa urais
kupitia tiketi ya chama cha Republican Donald Trump ameishambulia jamii
ya Wasomali wanaoishi katika jimbo la Minnesota nchini Marekani
,akiwalaumu kwa kueneza maoni yenye itikadi kali nchini humo.
Alitumia
mfano wa kisa cha shambulio la kisu lililotekelezwa na mhamiaji raia wa
Somalia mnamo mwezi Septemba katika mji wa St.Cloud ,akisema kuwa
wakaazi wa Minnesota wameteseka vya kutosha.
Bwana Trump ambaye
alikuwa katika ziara ya kampeni kabla ya uchaguzi wa Jumanne amesema
kuwa iwapo atakuwa rais atahakikisha kuwa wakaazi wa maeneo wanashauriwa
kabla ya wakimbizi kupelekwa ili kuishi.
Hivi ndivyo alivyosema Trump:
"Viongozi wetu wana ujinga
kiasi gani? Wana Ujinga kiasi gani kuruhusu mambo kama haya kutokea?
Hapa Minnesota mumekabiliwa na matatizo chungu nzima kutokana na ukaguzi
mbovu wa wakimbizi, huku idadi kubwa ya Wasomali wakiingia katika jimbo
hili bila wakaazi kufahamishwa,bila usaidizi wenu ama hata ruhusa.
Huku
wengine wakijiunga na kundi la wapiganaji wa Islamic State na kueneza
maono yao ya itikadi kali katika kila pembe ya nchi pamoja na dunia
nzima kwa jumla.
Kwa kweli ni vigumu kuamini na kila mtu anasoma
kuhusu mikasa inayotokea Minnesota...Mumeona kisa cha shambulio la kisu
katika eneo la St Cloud.
Serikali ya Trump haitasajili wakimbizi
bila usaidizi wa jamii ya eno hili.Hilo ndilo wanaweza kuwafanyia kwa
sababu mumeteseka vya kutosha."
Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika Jumanne 8 Novemba, 2016.
Post a Comment