Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknlojia Imewataka wanafunzi wa St. Joseph
waliohamishiwa katika chuo kikuu cha Dodoma kurudia mwaka kwa kile
kilichobainika kuwa na ujuzi na maarifa usiokidhi viwango vya chuo cha
Dodoma.
Wizara hiyo pia imesema kwamba watakaogomea uamuzi huo watatakiwa kurudi makwao .
Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, katika
mkutano wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU, Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako alisema, ni lazima wanafunzi hao
warudie mwaka kwani wamepimwa na kubainika kuwa na uwezo mdogo hivyo
hatua ya kuwataka kurudia mwaka ni nafasi ya pili kwao.
Prof. Ndalichako alisema, kwa sasa wizara yake inaandaa ripoti ya vyuo
vinavyofundisha chini ya viwango ambapo amesema mara tu baada ya
kukamilika ripoti hiyo, itatolewa na kwamba kwa wale wanafunzi ambao
vyuo vyao vimefungwa kwa kutokidhi vigezo ni lazima wapimwe kiubora ili
kupata wanafunzi watakao kidhi vigezo vya soko la ajira.
Aidha, Prof. Ndalichako ametoa onyo kwa wanafunzi ambao wamegushi
nyaraka mbalimbali ikiwemo za vifo vya wazazi wao ama ugonjwa na
kufanikiwa kupata mkopo wa elimu ya juu kwa njia ya udanganyifu kuwa
wizara hiyo inafanya uhakiki na pindi watakapo bainika hatua kali
zitachukuliwa dhidi yao.
Post a Comment