Na. Ahmad Mmow. Lindi
WAKALA
wa barabara(TANROADS) mkoani Lindi umefanikiwa kuiingizia serikali
jumla ya shilingi 118,668,200/= kutokana na faini ya kosa la kuzidisha
uzito kwenye magari.
Hayo
yalielezwa na meneja wa wakala wa barabara wa mkoa wa Lindi, Issack
Mwanawima, wakati wa kikao cha kawaida cha mkoa cha bodi ya barabara
kilichofanyika jana katika manispaa ya Lindi.
Mwanawima
alisema zoezi la kudhibiti uzito wa magari barabarani kwa kutumia
mizani zilizopo Mingoyo na Nangurukuru katika kipindi cha kuanzia mwezi
Machi hadi Oktoba mwaka huu, magari 153,681 yalipimwa.
Meneja
huyo alisema katika kipindi hicho magari 1163 yalikutwa yamezidisha
uzito kwa zaidi 5% inayoruhusiwa kisheria, hivyo zilitozwa kiasi hicho
cha fedha ambacho hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu
zilishalipwa.
"Takwimu
zinaonesha kuna ongezeko kubwa la magari katika barabara ya
Dar-eS-salaam, Lindi hadi Mtwara kutoka magari 75, 526 katika kipindi
cha Agosti 2015 hadi Februari 2016 na kufia gari 153,681 kwa mwaka huu
kuanzia kipindi cha mwezi Machi hadi Oktoba," alisema Mwanawima.
Mhandisi
Mwanawima alisema upimaji wa kutumia mizani ndogo inayo hamishika
uliohusisha magari yanayosafirisha saruji kutoka Mtwara kwenda
Dar-es-Salaam, ulifanyika hivi karibuni yalikuwa na uzito wa kawaida.
Hata hivyo upimaji uliofanyika katika maeneo ya Hotelitatu na
Kiranjeranje, ulibaini kuwa hata yanayobeba mawe ya madini ya
jasi(gypsum) yanayotoka migodini kwenda barabara kuu yalikutwa
yamezidisha uzito takribani mara mbili ya unaotakiwa kisheria.
Aidha
meneja huyo alibainisha kwamba katika mwaka wa fedha 2015/2016, mkoa
huu ulitengewa shilingi 1.35 bilioni kutoka fedha za maendeleo kwa ajili
ya kuzifanyia matengenezo barabara za mikoa zenye urefu wa kilometa
31.1.
Hata
hivyo kutokana na upungufu wa fedha kwa mwaka wa fedha 2014/2015 kiasi
hicho kilipunguzwa nakusababisha bajeti halisi kuwa shilingi
270.00milioni kwa mwaka wafedha wa 2015/2016.
Hata
hivyo hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu hakuna fedha zilizopokelewa kwa
miradi ya maendeleo. Mbali na hayo, mhandisi Mwanawima alisema jumla ya
shilingi 1.00 bilioni zimetengwa kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa
barabara ya Masasi, Nachingwea hadi Nanganga kwa kiwango cha lami. Ambapo nyaraka za zabuni zimeshawasilishwa makao makuu ya TANROADS katika mwaka wa fedha wa 2016/20017.
Kuhusu
barabara ya Nanganga, Ruangwa, hadi Nachingwea. Meneja huyo alibainisha
kuwa zimetengewa jumla ya shilingi 500.00 milioni kwa ajili ya kuanza
upembuzi yakinifu na sanifu wa kina. Ambapo zabuni kwa ajili ya kumpata
mhandisi mshauri ambazo tayari zimetangazwa, zimepangwa kurejeshwa
tarehe 13 mwezi Desemba mwaka huu.
"Kazi za usanifu wa ujenzi wa daraja la Lukuledi zilikamilika mwezi Julai mwaka 2014,na kwa mwaka huu wa fedha kiasi cha shilingi milioni 51.00 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi na zabuni kwa ajili ya kazi hiyo zimeshatangazwa," alisema Mwanawima.
"Kazi za usanifu wa ujenzi wa daraja la Lukuledi zilikamilika mwezi Julai mwaka 2014,na kwa mwaka huu wa fedha kiasi cha shilingi milioni 51.00 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi na zabuni kwa ajili ya kazi hiyo zimeshatangazwa," alisema Mwanawima.
Kwa
upande wake mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi ambae alikuwa
mwenyekiti wa kikao hicho, aliwataka wakurugenzi watendaji wa
halmashauri kufuatilia na kusimamia kwa karibu miradi ya ujenzi,
ikiwamo ya barabara zinazojengwa na halmashauri zao.
Post a Comment