0

Mamlaka wilayani Tarime mkoani Mara zimeendesha kubomoabomoa ya nyumba za makazi zilizojengwa kinyume na utaratibu katika eneo la kituo cha afya cha Kerende kilichopo Nyamongo wilayani Tarime ili kupisha upanuzi wa kituo hicho kitakachosaidia  kusogeza na kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa maeneo ya Nyamongo na mengine jirani.

Ni zoezi la kutekeleza mpango wa serikali wa kusogeza huduma za afya baada ya wakazi wa maeneo hayo kujenga na kuishi katika eneo hili kinyume na sheria.

Baada ya kumalizika kwa zoezi hilo lililodumu kwa zaidi ya masaa mawili serikali wilayani humo ikatoa neno kwa wananchi wa eneo hilo.

Post a Comment

 
Top