wachezaji wa timu ya ABC (Mpengele)fc waliovalia jezi nyeusi na blue timu ya Likongowele fc
Ikiwa leo novemba 9 katika matokeo ya ligi daraja la nne kulikuwa na mchezo kati ya timu ya Likongowele fc dhidi ya ABC (Mpengele)fc umemalizika kwa Likongowele fc kuibuka na ushindi wa magoli 7-4 mchezo uliochezwa katika uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
Magoli ya timu ya ABC FC yalifungwa na Nasoro Ndwekwike dakika ya 1,Abibu Mwite dakika ya 29 kwa mkwaju wa penaiti na dakika ya 48 huku goli la nne likifungwa na Bakari Machinda katika dakika ya 53.
Magoli ya timu ya Likongowele fc yalifungwa namo dakika ya 2 lililofungwa na Selemani Mpoto,Selemani Mwigama dakika ya 15 na dakika 47,Abasi Lipenga dakika ya 18 na dakika ya 86 na Abuu Matwiko dakika ya 84.
Post a Comment