Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la
Amina Hamisi (56) mkazi wa mtaa wa mahina kata ya Butimba Jijini
Mwanza, anashikiliwa na polisi baada ya kumlazimisha mjukuu wake wa kike
(jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka 7 kula kinyesi.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza
Kamishina Msaidizi wa Polisi Augustino Senga amedai kuwa tukio hilo
limetokea Novemba 11, mwaka huu ambapo mtoto huyo alikwenda chooni
kujisaidia na kushindwa kumwagia maji ili kuondoa kinyesi chake ndipo
bibi yake ili kumuadhibu alimuamuru kula kinyesi hicho kitendo ambacho
mtoto huyo alikitekeleza.
Baada ya tukio hilo kutokea raia wema
walitoa taarifa polisi ambao walifika eneo la tukio na kufanikiwa
kumkamata mtuhumiwa huyo.
Kamanda Senga ametoa wito kwa wakazi wa
jiii la Mwanza kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kudhibiti
vitendo vya kikatili hasa kwa watoto wadogo na kuongeza kuwa ukatili ni
kosa kisheria hivyo wananchi waache kufanya vitendo hivyo na watakao
bainika sheria itachukua mkondo wake.
Post a Comment