0
Matokeo ya ligi daraja la nne inayoendelea wilaya ya Liwale mkoani Lindi hapo jana novemba 8 kulikuwa na mchezo kali kati ya timu Polisi fc dhidi ya New generation mchezo uliopigwa uwanja wa Halmshauri ya Liwale.

Katika mchezo huu kwa kila upande ulikuwa mgumu sana kutokana na kila timu ilijipanga kutaka kupata ushindi au kutoa sare timu zote zilikuwa zinashambuliana katika kipindi chote cha dakika 45 kipindi cha kwanza lakini hakuna timu ilioweza kufumania nyavu ya mwezake.

Namo dakika ya 50 mchezaji wa Polisi fc,Lawrence Fusi aliipatia goli la kuongoza goli lililowanyanyua mashabiki wengi kwa mashabiki wengi waliiombea New generation ifungwe lakini matokeo yakabadilika baada ya Salumu Mkeyenge kusawazisha goli katika dakika ya 89 na matokeo yakawa sare kwa kufungana goli 1-1.

Kocha wa timu ya Polisi fc,Juma Lupia akizungumza na mwandishi wetu alisema timu yake ilicheza vizuri na wachezaji wake walifuata maelekezo aliowapa akiongeza katika mchezo ujao anatarajia kufanya vizuri nae kocha wa timu ya New generation,Saidi Kachepa alikiri mchezo huo ulikuwa mgumu huku akiwatupia lawama waamuzi wa mchezo huo na kuomba uongozi kuondoa kasoro kwa upande wa waamuzi.

Matokeo ya mchezo wa novemba 7 kati ya Sido fc dhidi ya Nangando fc ulimalizika kwa timu ya Sido fc iliweza kuibuka na ushindi mnono wa magoli 5-0


                    Mchezaji wa timu ya New generation akikimbia na mpira









                                mchezaji wa timu ya Polisi fc


                               Lango la timu ya Polisi fc lilivyoshambuliwa mara kwa mara

Post a Comment

 
Top