MKUU
wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, ameunda timu ya watu wanne
itakayofuatilia malipo ya fidia ya ardhi kwa ajili ya wananchi
walioondolewa katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.
Timu
hiyo imeundwa juzi wakati wa mkutano wa Mkuu huyo wa Wilaya na wananchi
hao. Mjema amesema timu hiyo itahusika pia kufuatilia ulipwaji wa
viwanja.
Akizungumza
kwenye mkutano huo, Mjema amesema ataunda timu nyingine ya watu sita
itakayochunguza tuhuma zilizotolewa na wakazi hao dhidi ya maofisa
waliodaiwa kuwa si waaminifu, wanaodaiwa kujilimbikizia viwanja na
kuwagawia wasiostahili.
Mjema
aliamua kuunda timu ya kufuatilia malipo hayo ya fidia baada ya maelezo
ya Mhandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), William
Shechambo mkutanoni hapo kutowaridhisha wananchi, kutokana na kutoonesha
lini watalipwa fidia na kupewa viwanja.
“Nitaunda
timu ya uchunguzi ya watu sita, yoyote atakayebainika kujinufaisha
tutamchukulia hatua kwa mujibu wa sheria na timu hii itapaswa kunipa
ripoti kabla ya Desemba 30, mwaka huu,” alisema.
Awali,
wananchi hao waliwasilisha malalamiko yao mbele ya Mjema na maofisa
wengine waliokuwepo kwenye mkutano huo ambao walidai kuwa hawafahamu
hatma ya maeneo yao yaliyochukuliwa na TAA kwa ajili ya utanuzi wa
kiwanja.
Wananchi
hao kutoka katika mitaa ya Kipunguni, Kigilagila na Pugu Kinyamwezi
walidai kuwa hawajalipwa fidia kama walivyoahidiwa na Serikali.
“Mkuu
wa Wilaya tunaomba kupewa viwanja vyetu kwa kuwa tunapata shida sana,
pia tumeingia kwenye mgogoro sisi kwa sisi,” alisema mmoja wa wananchi
hao aitwaye Gaudensia Pascal aliyedai kuwa nyumba zake tatu zilibomolewa
kupisha mradi wa upanuzi wa uwanja huo wa ndege na kwamba sasa ameingia
kwenye mgogoro na wanaye akituhumiwa kuuza eneo la nyumba zao
|
Post a Comment