Baada ya kushinda mechi mbili mfululizo huko kanda ya ziwa Timu ya Azam Fc imefungwa goli 2~1 dhidi ya Mbao ya mkoani Mwanza katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Ccm kirumba mkoani Mwanza.
Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Mbao walikuwa mbele kwa goli 1~0 goli lililofungwa katika dakika ya 29, kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Azam wakitafuta nafasi ya kusawazisha lakini mambo yalizidi kuwa magumu mnamo dakika ya 67 Mbao wakaandika goli la pili.
Goli pekee kwa upande wa Azam lilifungwa na Fransisco Zekumbawira katika dakika ya 78, mnamo dakika ya 86 kocha mkuu wa Azam Fc Zuben Harnandez aliondolewa kwenye benchi na mwamuzi Jacob Adondo baada ya kupewa maelezo kutoka kwa mwamuzi wa akiba Mathew Akrama.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.