Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Tarime mkoa wa Mara imebaini na
kuteketeza kwa moto mashamba saba ya bangi kwenye milima ya kijiji cha
Wegita wilayani humo ikiwa ni mkakati wa wilaya hiyo wa kutokomeza
kabisa kilimo hicho haramu ambacho kimekuwa kikiathiri nguvu kazi ya
taifa.
Ilituchukua mwendo wa karibu saa matatu kuupanda mlima wa Wegita ulioko
umbali wa kilometa nane ili kuyafikia mashamba makubwa ya bangi na
baadae kuyafyeka na kisha kuyateketeza kabisa mazao hayo.
Baada ya kumalizika kwa zoezi la kufafyeka na kuyachoma mashamba hayo
mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya
ya Tarime Bw. GLORIUS LUOGA akaelezea namna walivyofanikiwa kukomesha
ulimaji wa zao hilo.
Post a Comment