Shughuli zote zikiwemo za uzalishaji katika mgodi wa Tanzanite One
katika mji mdogo wa Merelani zimelazimika kusimama kwa zaidi ya saa sita
baada ya wakazi wa kijiji jirani cha Naisinyai kukusanyika katika lango
kuu la mgodi huo wakidai mwekezaji wa mgodi huo kukiuka makubaliano
muhimu waliyojiwekea wakati akichukua mgodi huo.
Wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali na silaha za jadi
Wakazi hawa waliojawa na jazba bila kujali wala kuogopa mabomu ya
polisi wanapiga kambi mbele ya lango kuu la kuingilia katika mgodi wa
Tanzanite one kuanzia Majira ya saa kumi alfajiri wakidai, mwekezaji
huyo kuwa ameshindwa kutekeleza kabisa hata moja ya makubaliano
waliyojiwekea wakati akichukua mgodi huo ikiwemo kuboresha huduma za
kijamii katika kijiji chao ambazo ni maji, elimu na afya.
Licha ya jeshi la polisi kuimarisha ulinzi katika eneo hilo wakati wote
wananchi hao walifanikiwa kuzuia wafanyakazi wote kutoingia wala kutoka
katika mgodi huo wakidai wanataka mwekezaji wa mgodi huo kufika eneo
hilo.
Inserts……
Channel ten inalazimika kumtafuta moja ya wakurugenzi wa mgodi huo na haya ndo maelezo yake.
Mgodi huo kwa sasa unamilikiwa na Kampuni ya wazawa ya uchimbaji wa
madini ya Sky Associates Group (LTD) ambayo ilinunua asilimia 50 ya hisa
zilizokuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Richland Resources ya Uingereza.
Post a Comment