0


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameanza ziara yake katika wilaya Kinondoni ambapo asubuhi ya leo amezungumza watumishi wa wilaya hiyo pamoja na kutoa baadhi ya maagizo.

Akiongea na watumishi wa wilaya hiyo, Makonda amewataka watumishi kufanya kazi kwa bidii huku akidai kuna baadhi ya watumishi wanashinda kwa waganga wakienyeji ili wasitumbuliwe.

“Kuna baadhi ya watumishi wanatembea na hirizi ili wasitumbuliwe, wakikutana na viongozi wao wanazibinya,” alisema Makonda. “Mimi ninachokitaka kutoka kwenu ni kuwatumikia wananchi wa chini,”

Pia Makonda amewataka wakuu wa wilaya wote kuanzisha kitengo maalum cha kisheria kitakacho tumika kutoa elimu kuhusu migogoro ya ardhi na kuwashauri wananchi kabla ya kupeleka malalamiko yao mahakamani na kuwaweka wazi kama kuna dalili ya kushinda au vinginevyo na kuwapa suluhisho la kudumu.

Katika hatua nyingine RC Makonda amemtaka DC Hapi na Meya wa Kinondoni Bernard Sita kufuatilia suala la vibali vya ujenzi na kuhakikisha vinatoka kwa wakati ili kuharakisha maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni DC Hapi amehaidi kuwashughukia watendaji wote watakao bainika kutowajibika kikamilifu ili kuchochea maendeleo.

Post a Comment

 
Top