0

Abiria wanaotumia usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam wameomba waendesha mradi UDA-RT kuimarisha ulinzi katika vituo vya mabasi hayo kutokana na kuibuka kwa tabia ya wizi katika vituo hivyo jambo ambalo hapo awali halikuwepo.

Wakizungumza na Channel Ten abiria hao wamesema wanadhani tatizo hilo limeibuka katika kipindi hiki kutokana na kusitishwa kwa daladala zinazotumia barabara ya morogoro hivyo vibaka waliokuwa wakifanya vitendo hivyo katika vituo vya daladala kuhamia katika vituo vya mbasi yaendayo haraka na kuwaibia abiria pindi wanapogombania kuingia kwenye mabasi hayo.

Licha ya kuwepo kwa wizi katika mabasi hayo baadhi ya abiria wameiomba mamlaka husika kukamiliksha miundombinu iliyosalia hususn kufunguliwa kwa milango ambayo kwa asilimia kubwa bado haijakamilishwa mashine za kukagulia tiketi hivyo kutoruhusu abiria kutumia milango hiyo jambo ambalo limekuwa na usumbufu kwani abiria hulazimika kutumia mlango mmoja na kupanga foleni ndefu.

Mmoja wa watumiaji wa usafiri ameshauri kuwepo kwa utaratibu wa kupanga foleni wakati wa kuingia kwenye mabasi hayo ili kuepuka msongamano na kuumizana wakati wa kugombania usafiri huo.

Post a Comment

 
Top