Mchezo wa ufunguzi ulikuwa kati ya Adamu Kejege (ado) dhidi
ya Miraji Bandu wote kutoka club ya Upendo boxing club Liwale ambapo wote
wakiwa na uzito wa kilo 58 na pambano lilimalizika kwa majaji kumtangaza
mshindi Adamu Kejege (Ado).
Kaimu Ligomba Vs Yassani Sadiki
Wapenzi wa mchezo wa masumbwi
wilayani Liwale mkoani Lindi jana
novemba 26 walishuhudia mpambano mkali wa kirafiki kati ya timu ya Upendo boxing
club Liwale mkoani Lindi na Black Mamba boxing
Mtwara mchezo uliopigwa ukumbi wa Rainer Club majira ya saa 4 usiku.
Kwa mujibu wa mratibu wa mpambano huo Amiri Kolela (poison) alisema mchezo huo una
lengo la kujenga na kudumisha masumbwi kwa kanda ya kusini.
Mchezo wa ufunguzi ulikuwa kati ya Adamu Kejege (ado) dhidi
ya Miraji Bandu wote kutoka club ya Upendo boxing club Liwale ambapo wote
wakiwa na uzito wa kilo 58 na pambano lilimalizika kwa majaji kumtangaza
mshindi Adamu Kejege (Ado).
Mpambano rasmi wa kwanza ulikuwa kati ya Muksini Kinderu (kilo
60) kutoka Liwale dhidi ya Juma Hamisi (kilo 65) kutoka Mtwara,mchezo huu
ulikuwa na raundi 6 na majaji wakatoa pointi kwa kumpa Muksini Kinderu pointi 78 na Juma
Hamisi pointi 84 hivyo mshindi aliweza kutangazwa Juma Hamisi kutoka timu ya
Black Mamba boxing Mtwara.
Mpambano wa pili iliwavutia sana mashabiki wa masumbwi ulikuwa kati ya Kaimu Ligomba (sebar) kilo 60
kutoka timu ya upendo boxing club Liwale dhidi ya Yassini Sadiki (kilo 60) kutoka timu ya Black Mamba boxing Mtwara mchezo uliokuwa na
raundi 6 pia.
Kwenye mchezo huu uliwafanya mashabiki kugawanyika kwa
kushangilia kila mmoja kwa upande wake bila kujali nani katokea wapi hali
iliyowafanya wapambanaji hao kucheza kwa umakini wa hali ya juu ili kuweza
kushinda.
Katika raundi ya kwanza kila mmchezaji alionekana kutega
mwezake lakini katika raundi ya pili hadi ya tano hali ya mchezo ulibadilika
kutokana na kila mchezaji kutaka kumsambaratisha mwezake mapema zaidi lakini
jitihada hizo ziligonga ukuta.
Raundi ya sita Kaimu
Ligomba alimpa makonde Yassini Sadiki na kuwafanya wapenzi wa masumbwi
kushangilia na baadae mwamuzi alimaliza
pambano na majaji wakaamua kutangaza
pointi.
Matokeo ya mchezo huo kwa mujibu wa majaji yalikuwa Yassini
Sadiki kutoka timu ya Black Mamba star alipata pointi 70 kutoka timu ya alipata
Upendo boxing club Liwale alipata pointi 75 hivyo mshindi katika mpambano huo
alikuwa ni Kaimu Ligomba.
Timu ya Upendo boxing club Liwale iliongozwa chini ya kocha
Amiri Kolela na kocha Mohamedi Jumbe kutoka
timu ya Black Mamba boxing
Mtwara.
Juma Hamisi akizungumza na mwandishi wetu alisema mpambano
dhidi ya Muksini Kinderu ulikuwa rahisi sana nae Mukisini Kinderu alisema
sababu ya kupelekea kupoteza pambano ilikuwa ni tofauti ya kuzidiwa uzito wa
kilo 6 yeye alikuwa na uzito wa kilo 60 na Juma Hamisi alikuwa na kilo 65.
Nae Yassini Sadiki alisema mchezo ulikuwa mzuri lakini
hakulidhika na maamuzi wa majaji lakini anajiamini kwa pambano lijalo atafanya
vizuri kwa upande wake Kaimu Ligomba alisema mchezo ulikuwa mzuri kutokana na
maandalizi mazuri ya muda mrefu aliongeza kusema anawaomba wadau wa masumbwi
kujitokeza kuweza kudhamini mapambano mengine.
ANGALIA VIDEO YA MPAMBANO ULIOKUWA MKALI NA WA KUSISIMUA
Post a Comment