Kumeripotiwa
shambulizi kubwa lililofanywa na wanamgambo kwenye kambi kubwa zaidi ya
wanajeshi wa Marekani ya Bagram nchini Afghanistan.
Jeshi linaloongozwa na NATO, lilisema kuwa watu wanne waliuawa na hadi 14 kuejruhiwa wakati kifaa kimoja kililipuliwa.
Maafisa
wanasema kwa huenda mlipuaji alikuwa ni mshambuliaji wa kujitoa mhanga,
ambaye alidanganya kuwa mfanyakazi wakati wafanyakazi walikuwa
wakiwasili katika kambi hiyo kwa shughuli za siku.
Kundi la Taliban linasema kuwa ndilo lilihusika. Hakuna taarifa zaidi kuhusu uraia wa wale waliouawa.
|
Post a Comment