Maafisa
watatu wa vyeo vya juu nchini Uganda wame hukumiwa kifungo cha miaka 10
gerezani kwa ufujaji wa karibu Dola milioni ishirini na tano,kutoka
hazina ya malipo ya uzeeni.
Mahakama
moja mjini Kampala imewapata maafisa hao na makosa ya kuelekeza malipo
ya uzeeni ya zaidi ya watu elfu mbili, katika akaunti zao za kibinafsi.
Mahakama
hiyo aidha imesema watatu hao wanaweza kukata rufaa dhidi ya huku hiyo.
Maafisa wengine watano wa vyeo vya chini katika hazina hiyo ya uzeeni,
pia wanatarajiwa kushtakiwa wa makosa sawia na hayo.
|
Post a Comment