Mkuu
wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Mary Tesha (kushoto), akipokea
cheti cha utambuzi kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini,
Joyce Fesso (kulia), wakati wa ufungaji wa Mafunzo kwa Wasanii wa Filamu
mkoani Mwanza yaliyoanza juzi Novemba 10 na kutamatika leo Novemba
12,2016 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Mhe.Tesha amemwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Na BMG
Na George Binagi-GB Pazzo
Mkuu
wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza,Mary Tesha, amemtaka Afisa
Utamaduni mkoani mkoani hapa, kuhakikisha maadhimio yaliyoafikiwa na
wasanii wa filamu mkoa wa Mwanza yanaanza hatua za utekelezaji ndani ya
siku saba.
Nje
ya hotuba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Tesha amesema Afisa Utamaduni mkoa
wa Mwanza, James Willium, kwa kushirikiana na maafisa utamaduni wa
halmashauri zote za mkoa wa Mwanza wanapaswa kuhakikisha wanatoa
mikakati ya utekelezaji wa maadhimio yaliyotolewa kwenye mafunzo hayo
ili utekelezaji huo uanze mara moja.
Miongoni mwa maadhimio saba ya wasanii walioshiriki mafunzo hayo ambayo yamewasilishwa na Mwakilishi
kutoka Chama cha Waongozaji wa Filamu mkoani Mwanza, Mwanaharusi Hela,
ni pamoja na uongozi (Serikali) wa mkoa wa Mwanza kusaidia upatikanaji
wa kituo cha sanaa (studio ya kisasa) kwa ajili ya kurekodia filamu na
vipindi vya runinga pamoja na kushirikishwa kwenye dhifa mbalimbali za
kimkoa na kitaifa ili kuonesha kazi sanaa zao.
Katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Sanaa Asilia, Mzee Fumbuki Lubasa, ametoa
bure kiwanja chenye ukubwa wa hekta 50 kwa 40 kilichopo Nyegezi Jijini
Mwanza ili wasanii wa filamu mkoani Mwanza wajengewe studio kwa ajili ya
kurekodia kazi zao ambapo Mfuko wa Pensheni wa PPF umeonesha nia ya
dhati ya kufadhiri ujenzi wake.
Zaidi
ya washiriki 300 wamepata mafunzo hayo ambapo Katibu Mtendaji wa Bodi
ya Filamu nchini, Joyce Fesso, amesema yamelenga kuwajengea weledi wadau
wa filamu wakiwemo waigizaji, waongozaji na wahariri, kutengeneza kazi
zenye ubora, kutambua majukumu ya bodi hiyo, hakimili na hakishirikishi
ili kukuza soko la filamu na hivyo kunufaika na kazi zao.
Meneja Mawasiliano kutoka Mamlaka ya
Mawasiliano nchini TCRA, Innocent Mungy (kushoto), akipokea cheti cha
utambuzi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha,
aliyemwakilishwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye ufungaji wa mafunzo kwa
wasanii wa filamu mkoani Mwanza hii leo.
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini,
Simon Mwakifwamba (kushoto), akipokea cheti cha utambuzi kutoka kwa Mkuu
wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, aliyemwakilishwa mkuu wa Mkoa wa
Mwanza kwenye ufungaji wa mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza
hii leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji mkoani
Mwanza, Ramadhan Mustapha (kushoto), akipokea cheti cha ushiriki kutoka
kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, aliyemwakilishwa mkuu wa
Mkoa wa Mwanza kwenye ufungaji wa mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani
Mwanza hii leo.
Mwakilishi kutoka Chama cha Waongozaji
wa Filamu mkoani Mwanza, Mwanaharusi Hela (kushoto), akipokea cheti cha
ushiriki wa mafunzo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha.
Mshauri wa sanaa
ya Filamu mkoani Mwanza ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti
wa Sanaa Asilia, Mzee Fumbuki Lubasa (kushoto), akipokea cheti cha
utambuzi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha.
Mzee Lubasa ametoa
bure kiwanja chenye ukubwa wa hekta 50 kwa 40 kilichopo Nyegezi Jijini
Mwanza kwa ajili ya wasanii wa filamu mkoani Mwanza kujengewa studio ya
kisasa kwa ajili ya kurekodia kazi zao.
Kushoto ni mmoja wa washiriki wa mafunzo
ya sfilamu yaliyoandaliwa na bodi ya filamu nchini, akipokea cheti cha
ushiriki kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani
Mwanza,Mary Tesha, akifunga Mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza
hii leo, kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
nchini, Joyce Fessoo, akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo ya
filamu mkoani Mwanza hii leo. Amesema lengo la mafunzo hayo ni
kuwajengea weledi wasanii wa filamu ili kutengeneza kazi bora.
Mshauri wa Utamaduni mkoani Mwanza,
James Willium, akizungumza wakati wa zoezi la ufungaji wa mafunzo kwa
wasanii wa filamu mkoani Mwanza hii leo
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akitoa mchango wake kuhusu uendelezaji wa soko la filamu mkoani Mwanza.
Mwakilishi kutoka Chama cha Waongozaji
wa Filamu mkoani Mwanza, Mwanaharusi Hela , akifuatilia mafunzo kwa
wasanii wa filamu mkoani Mwanza.
Msanii wa nyimbo za asili, Chifu
Mwananzengo (wa pili kulia) pamoja na wachezaji wake, akitoa burudani
kuhusu mkoa wa Mwanza kwenye ufungaji wa mafunzo kwa wasanii wa filamu
mkoani Mwanza hii leo
Washiriki wa mafunzo ya filamu mkoani
Mwanza wakifuatilia burudani kutoka kwa msanii wa nyimbo za asili, Chifu
Mwananzengo kutoka wilayani Kwimba hii leo
Washiriki wa mafunzo ya filamu mkoani Mwanza, wakifuatilia mada kwenye mafunzo hayo hii leo kabla ya mafunzo hayo kufungwa.
Washiriki wa mafunzo ya filamu mkoani
Mwanza, wakifuatilia mada kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
nchini, Joyce Fesso.
Picha ya pamoja
Bonyeza HAPA Kwa Habari Zaidi
Post a Comment