IKIWA ni baada ya waandaaji waTuzo za MTV EMA 2016
kumpokonya tuzo ya Best African Act mwanamuziki wa Nigeria, Wizkid na
kuahidi kumkabidhi Mbongo Fleva, Ali Kiba, kumekuwa na minonong’o mingi
na comment mbaya za mashabiki mitandaoni wakimshambulia kwa matusi na
kejeli Wizkid aliyepewa tuzo hiyo kimakosa.
Hali
hiyo imemfanya Alikiba afunguke na kuelezea namna anavyokerwa na baadhi
ya watu wanavyomshambulia Wizkid ilihali wao Kiba na staa huyo wote ni
wanamuziki na hawajawahi kugombana.
Kiba
hakukomea hapo, alienda mbali zaidi kwa kupost picha ya aliyopiga akiwa
na Wizkid na kuandika maneno haya kwenye akaunti yake ya Instagram.
“Sijafurahishwa
na ninachokiona kinaendelea kwenye mitandao ya kijamii, ninamkubali
sana wizkid kama msanii mwenzangu na kama mshabiki pia. Nimesikitishwa
sana na kushtushwa kuona watu wakimdhihaki Wizkid kwa maneno yasiofaa na
matusi, nataka kuwa muwazi tu naamini kuwa haya maneno yakijinga na
yasiyofaa hayahusishi na hayajatoka kwa mashabiki wangu wa kweli
kwasababu nafahamu wamekuwa wakijua jinsi gani namkubali Wizkid.
usizamishwe
na maneno ya mahater bro, hongera sana kwa kuwa mwaka huu umekuwa wa
mafanikio kwako, upendo wa dhati kutoka kwa mashabiki wangu wa kweli na
nchi ya Tanzania pamoja#KingKiba,”Ameandika Kiba.
|
Post a Comment