Pangani. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano,
January Makamba amesema mradi wa kudhibiti mabadiliko ya tabianchi
katika Mji wa Pangani uko mbioni kuanza.
January amesema mradi huo unalenga kudhibiti maji ili mjini huo ‘usimezwe’ na Bahari ya Hindi na kwamba utaanza hivi karibuni kwa gharamu ya Sh3 bilioni.
Waziri huyo amesema hayo wakati akikagua eneo litakalojengwa ukuta wa Mto Pangani ambalo limeathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.
January amesema Pangani inakabiliwa na changamoto ya kipekee kwa sababu dalili zinaonyesha mji huo unakwenda chini ya kina cha maji ya bahari.
Amesema mradi huo unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, ulibuniwa mwaka 2009 lakini haukuanza kwa sababu fedha zilikuwa hazitoshi.
Mkurugenzi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi amesema wameshakamilisha mchakato wa kupata mkandarasi wa nje na anahitajika mmoja tu kwa sababu atashirikiana na kampuni za ndani ya nchi.

Post a Comment