0

Mvomero. Baadhi ya mashamba ya mifugo yanayomilikiwa na Serikali, taasisi za dini na viongozi wa umma Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, wanadaiwa kuendesha mgomo baridi katika kushiriki uhakiki wa mifugo.

Hali hiyo imejitokeza kutokana na baadhi ya watendaji wa vijiji na maofisa mifugo kudai kuwa kazi hiyo imekuwa ngumu maeneo hayo na kutaja mashamba matatu yanayosumbua kuwa ni ya maereza ya vijana, Mbigiri na Kilimo.

Mashamba mengine yaliyotajwa ni Dakawa Farm Tec linalomilikiwa na Kanisa Katoliki na Shamba la Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood.

Ofisa Mifugo wa Wilaya ya Mvomero, Daniel Pangani amethibitisha kuwapo kwa usumbufu katika uhakiki huo hali iliyosababisha kuingilia kati na kuamua kuwasiliana na wamiliki.

“Kazi hii inafanywa na maofisa wetu ngazi za vijiji na kata, baada ya kufika katika mashamba hayo kuhakiki na kupiga chapa walikutana na vikwazo mbalimbali, hadi nilipoingilia kati,” amesema.

Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood amesema hakukataa kutoa ushirikiano bali taarifa za uhakiki hazikufikishwa kwa maandishi, hivyo kushindwa kushughulikiwa kwa wakati.

Post a Comment

 
Top