0


Mwanza. Ofisa Uhusiano wa Jiji la Mwanza,  Elirehema Kaaya amewataka watendaji kata na mitaa kuhamasisha usafi na mtu akayekataa atozwe faini ya Sh50,000.

Amesema viongozi hao wana wajibu wa kuhamasisha jamii kufanya usafi katika maeneo yao kwa kuwa hakuna mtu anayetakiwa kuishi sehemu chafu, vinginevyo wawapeleke mahakamani watakaokaidi.

Naye mkurugenzi wa jiji hilo, Kiomoni Kibamba amesema watendaji hao wanatakiwa kutimiza wajibu wao na kusimamia sheria kwa kutatua changamoto zinazojitokeza katika maeneo yao na kuacha kukaa ofisini kusubiri mishahara.

Pia, amewataka wananchi kufuata na kuzingatia kanuni za afya, kujenga na kutumia vyoo bora na kuacha kutiririsha maji machafu katika mitaro ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Nyamagana Thereza Mtesigwa amewaomba wananchi  kushirikiana na viongozi kutekeleza suala hilo.

Post a Comment

 
Top